Kipyegon atamani kuvunja rekodi kwa dakika nne

NAIROBI: MWANARIADHA wa Kenya Faith Kipyegon amesema anaamini kuwa atavunja rekodi ya dakika nne katika mbio zijazo ndiyo maana anaendelee na mafunzo makali.
Mkenya huyo alishindwa katika jaribio lake lililopangwa maalum mwezi Juni na kuwa mwanamke wa kwanza kupenya kizuizi cha dakika nne, akitumia dakika 4 na sekunde 06.42 katika jiji la Paris nchini Ufaransa.
“Lengo langu lilikuwa kuwa mwanamke wa kwanza kukimbia chini ya dakika nne. Ningesema sikufanya nilichotaka kufanya, lakini ilituma ujumbe kwamba inawezekana siku moja,” Kipyegon aliwaambia wanahabari katika mahojiano, kabla ya Mashindano ya Dunia ya mwezi ujao yatakayofanyika huko Tokyo.
Kijana huyo wa miaka 31, mshindi wa medali tatu za dhahabu katika Olimpiki, amesema tama zake za kutaka kufanikiwa zaidia kunamfanya awe anaamka asubuhi ili kufanya mazoezi kwa wakati.
“Ninaamini kutakuwa na mwanamke anayekimbia chini ya dakika nne katika kizazi kijacho au katika kizazi chetu. Nimefanikiwa sana, medali zote, Olimpiki na ubingwa wa dunia, lakini bado nina bidii, bado nataka kuonesha kuwa wanawake wana uwezo wa kufanya kile tunachopaswa kufanya katika ulimwengu huu, kwamba tumepata hii na tunahitaji kuifanya.”
Kipyegon asiyechoka alirejea ndani ya siku chache baada ya kukatishwa tamaa kwa jaribio lake la maili, na kuweka rekodi ya dunia ya mita 1500 ya 3:48.68 katika mkutano wa Prefontaine Classic Diamond League mjini Eugene.
Tokyo itakuwa michuano ya kwanza ambapo Riadha za Dunia zitasimamia mtihani mpya wa jinsia na Mkenya huyo amesema alikaribisha kuanzishwa kwake.
“Hili ni jambo jipya na sote tutakabiliana nalo. Ninatazamia kwa hamu.” Pia alikiri kuwa tayari alikuwa anakodolea macho kuelekea kwenye mbio za marathon.