EuropaKwingineko
Kipute robo fainali Europa leo

MECHI za kwanza za robo fainali ya michuano ya Europa zinapigwa leo.
Roma ya Italia itakuwa ugenini kuivaa Feyenoord ya Uholanzi kwenye uwanja wa de Kuip wakati Bayer Leverkusen ya Ujerumani itakuwa nyumbani kuikaribisha Union St. Gilloise ya Ubelgiji kwenye uwanja wa Bay.
Kibibi cha Turin, Juventus ya Italia itakuwa uwanja wake wa Allianz kukabili Sporting CP ya Ureno wakati Sevilla ya Hispania itakuwa mgeni wa Manchester United ya England kwenye uwanja wa Old Trafford.