Africa

Kipa wa Stellenbosch kuikosa tena Simba

DURBAN:GOLIKIPA namba moja wa Stellenbosch Sage Stephens ataendelea kuwa nje ya uwanja wakati klabu yake itakapowavaa wekundu wa msimbazi Simba SC kutoka Tanzania baada ya kutokuwa fiti kuwakabili wababe hao wa dar es salaam kwenye mechi ya mkondo wa pili wa nusu fainali ya Kombe La Shirikisho barani Africa (CAFCC)

Stephens alipata jeraha la nyama za kigimbi (calf strain) wakati kikosi chake kikufanya warm-up kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Zamalek ya Egypt huku nafasi yake katika mchezo huo ikichukuliwa na namba mbili wake Oscarine Masuluke.

Mwafrika Kusini huyo mwenye miaka 34 aliukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya AmaZulu April 15 lakini alitarajiwa kuwepo kwenye mchezo wa awali uliopigwa New Amaan Zanzibar jumapili iliyopita. Hata hivyo hakucheza kutokana na kutokuwa fiti vya kutosha kusimama kwenye milingoti mitatu.

Sasa ni rasmi hatakuwepo tena katika mchezo wa pili utakaopigwa katika uga wa Moses Mabhida uliopo jijini Durban nchini South Africa. Stellenbosch ni wageni wa michuano hii ikiwa ni msimu wao wa kwanza kwenye michuano ya CAF kwa ngazi za vilabu huku Simba wakiwa wanataka kuusimika ufalme wao barani humu kwa kufika fainali ya michuano hiyo pengine hataĀ kutwaaĀ taji.

Related Articles

Back to top button