Michezo MingineSoka La Ufukweni

Kikosi soka ufukweni COSAFA hiki hapa

WACHEZAJJI 16 wamechaguliwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya soka la ufukweni kitakachoshiriki mashindano ya Baraza la Vyama vya soka Kusini mwa Afrika(COSAFA).

Michuano hiyo itaanza Septemba 25, 2022 nchini Afrika Kusini.

Wachezaji waliochagaliwa watakaokuwa chini ya Kocha Boniface Pasawa na timu wanazotoka ni Adam Oseja(Mburahati), Ahmed Juma(Bubu), Ibrahim Hamidu(Huru), Shaban Hassan(Ihefu), Erick Manyama(KMC), Ismail Gambo(KMC), Juma Sultan(Huru) na Mtoro Nassoro(Msasani Mabingwa).

Wengine ni Stephano Nkomola(Green Warriors), Sadick Rajab(Green Warriors), Jaruph Rajab(Huru), Ibrahim Ibadi(Kijitonyama), Goodluck Gama(Friends of Mkwajuni), Yahya Tumbo(Huru), Stephano Mapunda(Mburahati) na Abdillah Mohamed(Ilala).

Related Articles

Back to top button