World Cup

Kikosi Brazil Kombe la Dunia hiki hapa

Kuelekea fainali za Kombe la Dunia zinazoanza tarehe 20 mwezi huu Qatar kocha wa timu ya taifa ya Brazil ‘Seleção Canarinho’, Adenor Leonardo Bacchi ‘Tite’ ametangaza orodha rasmi ya wachezaji 26 kwa ajili ya michuano hiyo.

Brazil ipi kundi G pamoja na Serbia, Uswisi na Cameroon na iwapo itaingia 16 bora huenda ikakutana na Ureno au Uruguay.

Seleção Canarinho ina nia ya kutwaa kwa mara ya sita kombe hilo miaka minne baada ya kupoteza katika nusu fainali kwa ubelgiji na 20 baada ya kushinda kwa mara ya mwisho fainali za Japan, 2002.

Orodha kamili ya wachezaji wa Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia 2022 na timu wanazotoka kwenye mabano ni kama ifuatavyo:

Magolikipa: Alisson Ramses Becker (Liverpool), Ederson Santana de Moraes (Manchester City) na Weverton Pereira da Silva (Palmeiras).

Mabeki wa Kati:Marcos Aoás Corrêa (PSG), Thiago Emiliano da Silva (Chelsea), Éder Gabriel Militão (Real Madrid) na Gleison Bremer Silva Nascimento (Juventus).

Mabeki wa Pembeni: Danilo dos Santos de Oliveira(Juventus), Daniel Alves da Silva (Pumas), Alex Nicolao Telles (Sevilla) na Alex Sandro Lobo Silva (Juventus).

Viungo: Carlos Henrique Casimiro (Manchester United), Fábio Henrique Tavares (Liverpool), Frederico Rodrigues de Paula Santos (Manchester United), Bruno Guimarães Rodriguez Moura (Newcastle), Lucas Tolentino Coelho de Lima (West Ham) na Éverton Augusto de Barros Ribeiro (Flamengo).

Washambuliaji: Neymar da Silva Santos Júnior (PSG), Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior(Real Madrid), Richarlison de Andrade (Tottenham), Raphael Dias Belloli (Barcelona), Gabriel Fernando de Jesus (Arsenal), Rodrygo Silva de Goes (Real Madrid), Antony Matheus dos Santos(Manchester United), Gabriel Teodoro Martinelli Silva (Arsenal) na Pedro Guilherme Abreu dos Santos (Flamengo).

Related Articles

Back to top button