EPLLigi Daraja La Kwanza

Kiasi cha pesa walichotumia United kwa Amorim

MANCHESTER:SAA chache tu baada ya kufutwa kazi na Manchester United, Ruben Amorim alionekana akitembea taratibu huku akiwa anatabasamu na kufurahi pamoja na mke wake, Maria, tukio lililogusa hisia za wengi mitandaoni. Hata hivyo, nje ya picha za furaha, utekelezaji wa uamuzi wa klabu umewalazimisha United kukabili bili kubwa ya kifedha kutokana na kusitisha mkataba wake.
Amorim aliingia Old Trafford Novemba 2024 akiwa na mkataba mpaka Juni 2027 na mshahara wa wastani wa paundi milioni 6.5 kwa mwaka, na alikuwa na takribani miezi 18 iliyosalia wakati alipofukuzwa United. Kulingana na uchambuzi wa gharama za usitishaji mkataba huo, United italazimika kumlipa Amorim takriban paundi milioni 12 (sh. bilionio 38 za kitanzania ) kwa kusitisha mkataba, bila kuhesabu malipo kwa wafanyakazi wake wa benchi na ada nyingine zinazoweza kuongezeka.
Ikumbukwe kuwa, klabu ililazimika kulipa ada ya karibu Paundi milioni 9.2 (takribani sh bilioni 29) kwa Sporting CP ili kuvunja mkataba wake na kumleata Manchester.
Ingawa ni chini ya mishahara ya baadhi ya wakufunzi wengine wa Ligi Kuu, bili hii bado ni kubwa sana kwa klabu, ukizingatia pia kumleta kocha mpya na utekelezaji wa mipango ya baadaye utatakiwa kulipwa pia.
 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button