Habari Mpya

Kaze amuelezea Kisinda, Mayele bado yupo Yanga

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema usajili wa Tuisila Kisinda utawarahisishia kutetea mataji yao yote mawili ya ndani na kufanya vizuri kimataifa.

Akizungumza na Spotileo, kocha huyo amesema anajua uwezo wa mchezaji huyo ndio maana anaamini atakuwa na mchango mkubwa katika kutimiza malengo ya timu msimu huu.

“Nimefanya kazi na Kisinda karibu msimu mzima hapa ndio alikuwa mchezaji wangu tegemezi katika kuanzisha mashambulizi na napenda kasi yake ndio maana nikasema atakuwa ni msaada mkubwa kwetu,” amesema Kaze.

Amesema Yanga ina hazina kubwa mawinga wakiwemo Bernard Morrison, Jesus Moloko na Dickson Ambundo hivyo kutoa nafasi pana ya kuchagua mchezaji wa kuanza.

Kisinda amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na RS Berkane ya Morocco.

Fiston Mayele(Kulia) akiwa ameshika mkataba

 

Wakati huo huo Yanga imetangaza kuwa mshambuliaji Fiston Mayele ataendelea kubaki klabu hiyo baada ya kusaini mkataba mpya.

Related Articles

Back to top button