Karia: Tutapandisha hadhi michuano ya Cecafa

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Wallace Karia amesema wanataka kuyafanya mashindano ya Kagame kuwa makubwa zaidi kuanzia msimu ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Leo Karia alisema wanafanya mazungumzo na wadhamini mbalimbali namna gani waboreshe kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa kiwango kikubwa.
Alisema katika kuhakikisha yanapewa kipaumbele kikanda amehimiza vyama vya soka kila nchi kuyaingiza kwenye kalenda zao ili kila mwaka mwezi kama huu yawe yanafanyika kuzisaidia timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa kujiweka imara.
“Sisi tumeyaingiza kwenye kalenda, nimewaagiza vyama vya soka nchi nyingine zote kuyaingiza haya mashindano kwenye kalenda zao, kila mwaka timu zijiandae mapema kushiriki,”alisema Karia ambaye pia, ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Alisema mwakani mashindano hayo yataanzia hatua ya robo fainali kuzipa nafasi timu kujiandaa na mashindano mengine ikiwemo Ligi Kuu.
Aliwashukuru wadhamini wa mashindano hayo msimu huu wakiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, wa Rwanda Paul Kagame na Mamlaka ya Bandari Tanzania Dar Port akisema yamekuwa yenye ushindani.
Kesho ni na nusu fainali ya Cecafa ambapo APR ya Rwanda itachuana na Al Hilal ya Sudani kwenye Uwanja wa KMC huku Al Wadi ya ikitarajiwa kuchuana na Red Arrows ya Zambia Uwanja wa Azam Complex Chamazi.