Nyumbani

Karia Aongoza Ujumbe wa Tanzania Vienna

DAR ES SALAAM:RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ametoa shukrani kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa washiriki wa Warsha ya kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu duniani. Warsha hiyo inahusisha nchi wanachama wa UEFA na CAF na inaendelea mjini Vienna, Austria.
 
Karia amesema kuwa ni heshima kwa Tanzania na kwa TFF kushiriki pamoja na mashirikisho mengine kutoka Afrika na Ulaya.
 
“Ni furaha kuwa miongoni mwa washiriki kwa sababu mijadala mingi inasaidia sana na inatupa data za kuweza kuendeleza mpira wa miguu nchini kwetu,” amesema.
 
Aidha, Karia amesema kuna haja ya warsha za aina hiyo kuendelea kutolewa mara kwa mara ili kutoa maarifa yatakayosaidia katika shughuli za kila siku za kuendeleza soka.
 
Nchi zinazoshiriki kwenye warsha hiyo ni Finland, Moldova, Wales, Austria, na Georgia kutoka UEFA, pamoja na Gabon, Morocco, Senegal, Tanzania na Cameroon kutoka CAF.

Related Articles

Back to top button