La Liga

“Kama sio kocha Flick ningeondoka Barca” – Raphinha

BARCELONA: WINGA wa mabingwa wa LaLiga FC Barcelona, Raphinha amefichua kuwa alikuwa amefikiria kuondoka katika klabu hiyo lakini aliamua kusalia baada ya kupigiwa simu na kocha wa kikosi hicho Hansi Flick, ambaye alimpa nafasi nyingine mpya ya kuonesha uwezo wakie uwanjani.

Raphinha amesema katika mahojiano na gazeti la kila siku la SPORT la nchini Hispania kuwa Kocha Hansi Flick amekuwa kama baba yake mlezi na kabla ya ujio wake klabuni hapo. Kabla ya Flick kuwasili na kumshawishi abaki hakuwa anaona maisha yake ya soka yakiendelea katika kikosi cha wababe hao wa Catalonia.

“Sikuwa mimi tu, watu wengi walitaka niondoke hapa, mashabiki na labda bodi haikufurahishwa na nilichokuwa nakifanya, mimi ni mtu wa kufikiria kuwa usipokaribishwa mahali ni bora usiwepo, Kusema kweli, sikutarajia. Malengo niliyokuwa nayo yalikuwa chini ya takwimu hizi. Umekuwa msimu bora zaidi wa maisha yangu.” – alisema

“Kocha alinipigia simu na kuniambia kwamba ananitegemea. Simu hiyo ilikuwa muhimu sana kwa sababu ilibadilisha mtazamo wangu kwa sababu Mtu pekee ambaye angeweza kunizuia ni yeye na akafanya hivyo.” aliongeza

Raphinha alikuwa na wakati mgumu chini ya kocha Xavi Hernandez, akisema Mhispania huyo na wasaidizi wake hawakuonesha imani kubwa katika uwezo wake. Lakini tangu kuwasili kwa Flick amekuwa nan amba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza ikilinganishwa na mara 17 tu kwenye LaLiga msimu wa 2023-24 chini ya Xavi.

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 28 alichangia pakubwa katika mbio za Barcelona za kuwania ubingwa wa LaLiga, akichangia mabao 34 na asisti 25. Hata hivyo, Raphinha alisema hata hakufikiria kufikia takwimu hizo mwanzo wa msimu. Tayari winga huyo ameongeza mkataba kusalia Barca hadi Juni 30 2028.

Related Articles

Back to top button