Ligi KuuNyumbani

Kagera Sugar kujitathmini

UONGOZI wa timu ya Kagera Sugar umesema utakutana na benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu Francis Baraza kutathmini hali ya mwenendo wa timu hiyo kufuatia vipigo viwili mfululizo Ligi Kuu Tanzania Bara hivi karibuni.

Akizungumza na Spotileo, Katibu Mkuu wa timu hiyo Ali Masoud amesema bado uongozi haujamua juu ya kocha huyo licha ya matokeo waliyokuwa nayo.

“Hatuwezi kukurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahihi mpaka tufahamu shida inayosababisha timu kufanya vibaya. Ni baada ya hapo ndio tutamuita kocha kuzungumza naye,” amesema Masoud.

Amesema uongozi haufurahishwi na mwenendo wa timu ingawa kwa kushirikiana na benchi la ufundi wanapambana ili kumaliza changamoto hizo.

Timu hiyo ilipoteza nyumbani dhidi ya Singida Big Star kwa mabao 2-1 Oktoba 21 kisha ugenini dhidi ya Namungo kwa mabao maba 2-1 Oktoba25.

Kagera Sugar inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 9.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button