Ligi Ya WanawakeNyumbani

JKT Queens kuendeleza makali SLWPL leo?

RAUNDI ya nane ya Ligi Kuu ya soka ya wanawake Tanzania Bara inaendeleo kwa michezo mwili Dar es Salaam na Iringa.

Wakali wa ligi hiyo JKT Queens ambaye ni timu pekee haijapoteza mchezo hadi sasa itakuwa mwenyeji wa Fountain Gate Princess kwenye uwanja wa Maj Gen Isamuhyo, Dar es Salaam.

JKT Queens ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 17 baada ya michezo 7 wakati Fountain Gate Princess inashika nafasi 4 ikiwa na pointi 16 baada ya michezo 7.

Ceasiaa queens itakuwa mgeni wa Mkwawa Queens kwenye uwanja wa Chuo cha Mkwawa mkoani Iringa.

Katika mchezo mmoja wa ligi hiyo uliopigwa Februari 7 kwenye uwanja wa Uhuru Yanga imeichapa The Tiger Queens mabao 5-0 huku Blessing Nkor wa Yanga akifunga mabao 3.

Related Articles

Back to top button