Africa
JKT Queens karata muhimu Afrika

KLABU ya JKT Queens leo inashuka dimbani katika mchezo muhimu wa mwisho wa makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake dhidi ya Sporting Casablanca kwenye uwanja wa San-Pédro, Ivory Coast.
JKT Queens iliyopo kundi A ilipoteza mshezo wa kwanza kwa mabao 2-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns kabla ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Athletico Abidjan.
Katika mchezo mwingine leo Mamelodi Sundowns itaivaa Athletico Abidjan.