
MSAFARA wa watakaohusika kwenye uzinduzi wa jezi mpya za klabu ya Simba kwa msimu wa 2023/2024 umeondoka Dar es Salaam kwenda mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya tukio hilo la Julai 21,2023.
Mapema leo Julai 18, 2023 Meneja wa habari na wasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amechapisha katika ukurasa wake wa instagram taarifa ya kuanza safari ya kuelekea mlima Kilimanjaro.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi mhandisi Hamad Masauni ni mmoja ya watakaohusika kwenye tukio hilo na ameanza pia safari ya kuelekea kwenye shughuli hiyo.
Ikumbukwe Simba walitangaza kuwa Julai 21, 2023 watatambulisha rasmi jezi zao katika kilele cha mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza Mlima kilimanjaro kupitia tukio hilo.