Ligi Kuu

Hatma ya Prince Dube kujulikana leo

HATMA ya mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Prince Dube, kuhusu uwezekano wa kushiriki mchezo mkubwa wa Kariakoo Derby dhidi ya Simba, inatarajiwa kujulikana leo Ijumaa ya Juni 20, baada ya kufanyiwa vipimo vya kina kufuatia jeraha la nyama za paja.

Daktari wa Yanga, Moses Etutu, amethibitisha kuwa maendeleo ya mchezaji huyo raia wa Zimbabwe yanaendelea vizuri, huku matibabu yakiendelea tangu alipopata maumivu katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Jumatano, Juni 18, jijini Mbeya.

“Dube alipata maumivu ya nyama za paja la kushoto. Tulianza kumpatia matibabu mara baada ya mchezo na hali yake inaendelea kuimarika.

Tunatarajia Ijumaa tutakapowasili Dar es Salaam atafanyiwa vipimo vya kina ili kubaini ukubwa wa tatizo,” amesema Dk Etutu.

Ameongeza kuwa matokeo ya vipimo hivyo ndiyo yatatoa mwanga kama Dube atakuwa sehemu ya kikosi kitakachovaana na Simba katika mechi hiyo ya kihistoria ambayo pia inaweza kuwa ya uamuzi wa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga, ambao wanaendelea kupambana kusaka mataji mawili yaliyosalia, wamesaliwa na michezo miwili ya ligi dhidi ya Dodoma Jiji FC na Simba SC, kabla ya kukamilisha msimu kwa kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Singida Black Stars.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button