Nyumbani

Hatma ya Dabi ya Kariakoo imeamuliwa Ikulu?

RAIS Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Klabu kongwe za soka nchini, Simba SC na Yanga SC, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Ujumbe wa Klabu ya Simba umeongozwa na Mwenyekiti wa sasa Murtaza Mangungu, akifuatana na Mwenyekiti wa zamani Hassan Dalali, Mjumbe wa Bodi na Mbunge, Rashid Abdallah Shangazi, na Hassan Hasanoo.

Kwa upande wa Klabu ya Yanga, ujumbe umeongozwa na muwekezaji Gharib Said Mohamed (GSM), Mkamu wa Rais Arafat Haji, na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo, Andrew Mtime.

Katika picha ya pamoja ilipigwa mara baada ya mazungumzo hayo, Rais Samia ameonesha nia thabiti ya kuona michezo ikichochea mshikamano wa kitaifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button