Harry Kane mfalme mpya England

MUNICH: Harry Kane amejitambulisha rasmi kama mfalme mpya kwenye soka la England baada ya kuweka rekodi mpya katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kane amekuwa kuwa raia wa kwanza wa England kufunga mabao 33 kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya katika ushindi wa mabao 9-2 wa Bayern Munich mbele ya Dynamo Zagreb.
Awali rekodi hiyo ilishikiliwa na Mwingereza mwenzake mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney aliyekuwa na mabao 30
Harry Kane pia anakuwa Mwingereza wa kwanza kufunga mabao manne katika mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya pia mchezaji wa kwanza kufunga hattrick kutokana na penalti.
Matokeo ya mechi za jana
Bayern Munich 9-2 Dinamo Zagreb
Real Madrid 3-1 VfB Stuttgart
AC Milan 1-3 Liverpool
Sporting Lisbon 2-0 Lille OSC
Juventus 3-1 PSV Eindhoven