Mastaa

Harmonize Amjia juu Baba Levo

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, amemjibu vikali msanii mwenzake Baba Levo baada ya Baba Levo kum-post na kudai kuwa Diamond Platnumz ndiye “baba” yao na mtu aliyewainua wasanii wengi nchini.

Katika sehemu ya maoni kupitia ukurasa wa Instagram, Harmonize ameibua gumzo baada ya kumrushia maneno mazito Baba Levo, akisisitiza kuwa kauli za Baba Levo kuhusu Diamond hazana mashiko na hazina uhalisia.

Katika ujumbe wake mrefu, Harmonize ameandika:“Wewe binafsi hakusaidii chochote zaidi ya kupiga naye picha… umekuwa ukilalamika kila tukikutana kasino, ndiyo kauli yako ya kuomba hela ndugu mbunge. Ipo siku utasema nani alikusaidia pesa za kampeni.”

Akiendelea kumshambulia, Harmonize alihoji kuhusu msaada wa matibabu kwa msanii Anjella, akimtaka Baba Levo awe muwazi kuhusu alichowahi kumsaidia:

“Tuongee kuhusu Anjella, ulikuwa mstari wa mbele kusema simtibii, mmempeleka hospitali anaendeleaje? Nyimbo na Zuchu vipi, Ibraah mbona hamuendelei ku-promote ngoma zake?”

Harmonize alituhumu kuwa Baba Levo na wenzake wamekuwa wakitumia wasanii wadogo kwa faida zao binafsi:

“Lengo lenu ilikuwa kushughulika na kupita madogo… yeyote anaye-support upuuzi wenu. Nawaahidi, kama nilishindwa kufa kipindi mlichosambaza uongo sikutetereka, kilichobaki ni nyinyi kuleta drama tu.”

Amemalizia, Harmonize ameandika kuwa Mungu ndiye shabiki namba moja wa Konde Gang, akisisitiza kwamba hapangiwi na presha za mitandaoni.

Related Articles

Back to top button