Kwingineko

Hapatoshi fainali ya WAFCON

RABAT: KOCHA wa timu ya Taifa ya wanawake ya Morocco, Jorge Vilda amesema kikosi chake kiko tayari kumenyana na timu ya taifa ya wanawake Nigeria katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake itakayopigwa leo Jumamosi mjini Rabat, huku wakiwa na matumaini makubwa ya kubeba kombe hilo.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 44, ambaye aliiongoza Hispania kufanikiwa kwenye Kombe la Dunia la Wanawake mwaka 2023 kabla ya kuondoka kwake kwa utata kufuatia kashfa ya kubusu  ya Luis Rubiales, anaamini kuwa simba wake wa Atlas wameonesha ujasiri wa kisaikolojia unaohitajika kutwaa taji la kwanza la bara la Morocco.

Uteuzi wa Vilda na Morocco ulikabiliwa na maoni tofauti kutokana na mazingira ya kuondoka kwake huko Hispania, ambapo aliachwa katikati ya mzozo wa rais wa shirikisho la wakati huo Rubiales dhidi ya mchezaji Jenni Hermoso.

Hata hivyo, kocha huyo amefanikiwa kuweka umoja kwa wachezaji anaowafundisha sasa wa Morocco na amesifu maendeleo ya timu ya Nigeria, na kukiri kuimarika kwao katika kipindi chote cha shindano hilo, akisema, “Nigeria imeonesha kuimarika sana kupitia mashindano hayo na kushinda timu ngumu sana, lakini tutakabiliana nazo bila timu hofu.”

Super Falcons hawajawahi kupoteza fainali katika majaribio tisa yaliyopita na wanatafuta taji la 10 ilikuongeza rekodi yao.

“Nigeria ina wachezaji wenye nguvu za kimwili na wachezaji bora sana kwa sifa zao binafsi. Wanacheza ligi kubwa na wameshinda kombe mara nyingi.”

Kocha huyo alifichua wasiwasi wake kuhusu jeraha kabla ya mechi ya fainali, akithibitisha kwamba mshambuliaji Fatima Tagnaout alikuwa na shaka na alikabiliwa na mtihani wa utimamu wa mwili siku ya Ijumaa wakati wa mazoezi yao ya mwisho.

Iwapo Vilda ataiongoza Morocco kupata ushindi, ataweka historia nyingine baada ya kubeba Kombe la Dunia la Wanawake akiwa na Uhispania.

Related Articles

Back to top button