Kwingineko

Twiga Stars njia panda kufuzu Olimpiki 2024

TIMU ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake(Twiga Stars) imepoteza mchezo wa kwanza raundi ya tatu wa kufuzu michezo ya Olimpiki Paris 2024 baada ya kuchapwa mabao 3-0 na timu ya taifa ya Afrika Kusini(Banyana Banyana).

Mchezo huo umefanyika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo wa marudiano utafanyika Februari 27 kwenye uwanja wa Mbombela uliopo Jimbo la Mpumalanga, Afrika Kusini.

Michezo ya Olimpiki ya Paris imepangwa kufanyika kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, 2024.

FULLTIME

TWIGA STARS 🇹🇿 0️⃣-3️⃣ 🇿🇦 BANYANA BANYANA

Jermaine Seoposenwe 10′
Thembi Kgatlana 57′
Hildah Magaia 86′

Related Articles

Back to top button