Kwingineko

Hansi Flick:Fainali 8, makombe 8

JEDDAH:HANSI Flick anaendelea kujijengea heshima ya kipekee kwenye dunia ya soka, hasa linapokuja suala la fainali. Popote anapofika, akifika hatua ya mwisho, mara nyingi hadithi huwa ile ile,Flick anatoka na kombe. Kocha huyo sasa ameweka rekodi ya kushangaza baada ya kushinda fainali nane kati ya nane alizowahi kusimamia katika maisha yake ya ukocha.
Ushindi wake wa hivi karibuni kwenye Supercopa de España 2026 umeongeza uzito zaidi kwenye jina lake, na kuifanya rekodi yake ibaki safi kabisa. Fainali nane, mataji nane. Hakuna aliyewahi kumfunga Flick kwenye mchezo wa kuamua bingwa.
Rekodi hiyo inabeba mataji makubwa kabisa aliyoyatwaa katika ngazi ya juu, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia la Klabu, UEFA Super Cup, DFB Pokal, DFL Supercup, Supercopa de España pamoja na Copa del Rey.
Kinachomtofautisha Flick si makombe tu, bali namna timu zake zinavyoingia fainali zikiwa na utulivu, umakini na njaa ya kushinda. Kila fainali kwake imekuwa kama mtihani anaoujua tayari jibu lake. Ndiyo maana jina lake linazidi kuandikwa kwa wino mzito kwenye vitabu vya makocha wakubwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button