Tetesi

Guardiola: Tunamhitaji Gundo

BARCELONA na Arsenal huenda zikapigwa na butwaa baada ya taarifa kuwa kocha wa Man City, Pep Guardiola ana matumaini ya kiungo Ilkay Gundogan kubaki City.

“Nafahamu Barcelona wanavutiwa na kumsajili Gundo, ila na sisi tunahitaji abaki matumaini yangu atabaki na sisi.” Amesema Guardiola.

Kocha huyo amesema kama Barca wakifanikisha usajili huo watakuwa wamepata mchezaji mzuri.

Mkataba wa Gundogan umemalizika msimu huu, bado mchezaji huyo hajafanya maamuzi yoyote juu ya mustakabali wake.

Related Articles

Back to top button