Kwingineko

Guardiola aimezea mate FIFA CWC

MANCHESTER:KOCHA mkuu wa Manchester City Pep Guardiola ameonesha hamu yake ya kucheza kwenye kombe la FIFA la dunia la vilabu 2025(FIFA CWC) linalotarajiwa kuwasha moto kuanzia tarehe 14 mwezi Juni hadi Julai 13 mwaka huu nchini Marekani.

Akizungumza na DAZN Football meneja huyo mwenye historia ya kipekee kwenye soka la England amesema mashindano hayo ni fursa mpya ya kupata ladha mpya ya soka kutoka maeneo tofauti kama Afrika, Amerika Oceania na Asia akisema klabu yake iko tayari kwa changamoto mpya.

“Kwa kawaida ninapoanza shindano huwa sina yale mawazo ya ooh tunaenda kushinda, ni hatua kwa hatua kujiimarisha alafu tutaona itakavyokuwa. Mimi naona ni fursa na naitaka” – Amesema

“Kila kinachotokea leo kwenye mpira ni kipya hata kwenye hizi ligi za nyumbani kuna mameneja tofauti tamaduni tofauti, staili na njia mpya za uchezaji kikubwa ni kucheza na timu tofauti kutoka maeneo tofauti kama Oceania, Asia, America Kusini na mengineyo”

“Shindano hili ni jipya na ndo mpira ulivyo si ndio, huwezi kubaki na staili zilezile ni lazima upate mtazamo mpya, ukutane na aina mpya ya wachezaji na huo ndio uzuri wa utamaduni wa soka”

Manchester City itatupa karata yake ya kwanza dhidi ya klabu kutoka Morocco ya Wydad Athletic Club maarufu kama Wydad Casablanca, kisha Al Ain ya UAE na kumaliza na mabingwa wa zamani wa Serie A ya Italia Juventus.

Related Articles

Back to top button