Filamu

Govinda atakiwa na mkewe afanane na Rambo

INDIA: MKE wa Govinda, Sunita Ahuja amefichua kwamba alimwomba mwigizaji huyo kupoteza angalau kilo 20 na kufanya kazi zaidi katika filamu ili afanane na mcheza filamu za mapigano Sylvester Stallone ‘Rambo’.

Muigizaji wa Bollywood Govinda amekuwa mbali na filamu kwa muda mrefu sasa.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na Instant Bollywood, mke wa muigizaji huyo, Sunita Ahuja amesema alimsihi mno mumewe apunguze uzito afanane na Rambo ili arejee kuigiza filamu zake kama zamani.

Mke huyo anasendelea kueleza: “Miaka kadhaa Govinda aliwahi kuniahidi kuwa angekuwa kama muigizaji anayempenda zaidi, Sylvester Stallone Rambo.

Sunita ameendelea kusisitiza kwamba; “Sijawahi kugombana na Govinda juu ya kitu chochote isipokuwa jambo moja tu kwamba nataka aanze kufanya kazi tena za utengenezaji wa filamu anawakosea mashabiki wake wengi duniani kote.

“Nilimwambia apunguze uzito, apunguze angalau kilo 20. Takriban miaka 6 hadi7 iliyopita, naendelea kumwambia nataka arudi kazini sababu aliniahidi, atakuwa kama Rambo.”

“Nilimwambia, ‘Haionekani kuwa inawezekana katika maisha haya, na katika maisha yanayofuata, sitaki uwe mume wangu au mwanangu.”

Sunita aliongeza, “Yeye haoni uzito wala hafanyi sinema. Ninamwambia kwamba wewe ni muigizaji mashuhuri lakini unapoteza muda wako kwa sababu ya watu wanne ambao unakaa nao. Hawakufundishi mambo mazuri takataka tu. Kaa na watu wazuri na ufanye kazi nzuri.”

Sunita na Govinda walifunga pingu za maisha hata kabla ya Govinda kuwa supastaa wa Bollywood. Wenzi hao waliweka ndoa yao kuwa siri, wakiikubali hadharani tu baada ya kuzaliwa kwa binti yao Tina. Wameoana kwa takriban miaka 38 na pia wana mtoto wa kiume, Yashvardhan Ahuja, ambaye yuko tayari kufanya tafrija yake ya kwanza ya Bollywood hivi karibuni na filamu ya ‘Sai Rajesh

Related Articles

Back to top button