World Cup

Ghana, Tunisia kuikabili Brazil

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Brazil(CBF) limesema timu ya taifa ya nchi hiyo ‘Seleção Canarinho’ itakabliana na Ghana na Tunisia mwezi ujao katika michezo ya kirafiki ya maandalizi ya Kombe la Dunia.

Wachezaji 26 wameitwa kwenye kikosi cha Seleção Canarinho kitakachoshiriki michuano hiyo ya dunia baadaye mwaka huu.

CBF imesema katika tovuti yake kwamba mechi hizo za maandalizi zifanyika barani ulaya Septemba 23 na 27 katika viwanja ambavyo bado havijatajwa.

Septemba 9 Kocha Mkuu wa Brazil, Adenor Leonardo Bacchi maarufu Tite atatangaza wachezaji watakaocheza michezo hiyo ya kirafiki.

Brazil inaongoza duniani kwa viwango vya soka na ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kutwaa Kombe la Dunia ambalo mashindano yake yatafanyika Qatar kuanzia Novemba 20 hadi Desemba 18, 2022.

Brazil imepangwa kundi G pamoja na Serbia, Uswisi na Cameroon huku mchezo wake wa kwanza ukiwa Novemba 24.

Ghana itakuna na Korea Kusini, Ureno na Uruguay katika kundi H na huenda ikakutana na Brazil katika 16 bora.

Nayo Tunisia iko kundi D pamoja na Australia, Denmark na mabingwa watetezi, Ufaransa.

Related Articles

Back to top button