Filamu ya marehemu Charles Ouda kuoneshwa kesho
NAIROBI: BAADA ya Tamthilia ya ‘Pepeta’, kuonesha mafanikio makubwa nchini Kenya, tamthilia mpya mahususi kwa watu wazima inayoiywa ‘4 Play’ inatarajiwa kuanza kuoneshwa kwa mara ya kwanza nchini humo.
Tamthilia hiyo imepewa daraja 18 inaangazia maisha na changamano ya wanaume wanne wanaopitia urafiki, mapenzi wakiwa wanaishi katika jiji la Nairobi.
Tamthilia hiyo ndiyo mradi wa mwisho wa muigizaji na mwandishi wa miswada, Charles Ouda, ambaye alifariki dunia Februari 3, 2024 akiwa na miaka 38 ambapo hadi leo familia yake haijaeleza kifo chake kilitokana na nini.
Tamthilia hiyo inayooneshwa kwa mara ya kwanza tarehe 21 Novemba 2024. Ikiangazia mfululizo wa mapambano na ushindi wa wanaume kusawazisha machafuko binafsi, uaminifu na tamaa.
Waigizaji wakuu ni pamoja na waigizaji wakongwe Daniel Weke (Mali), Elsaphan Njora aliyeteuliwa na AMVCA (Kati Kati, Twende), Maina wa Ndungu (Kina, Volume) na mshindi wa Tuzo ya Kalasha Bilal Wanjau (Faithless).
Wengine ni Edu na Michael marafiki wanaopitia safari isiyotabirika ya maisha ya jiji. Wanaungana na Patricia Kihoro, mwimbaji na mwigizaji Habida Moloney (Zari), na Tracy Macharia (Big Girl Small World).
Tamthilia hiyo imetayarishwa na James Kombo wa CJ3 Entertainment, imeongozwa na Mwangi Rurengo (Pepeta), Janet Chumbe (Faithless) na Mkaiwai Mwakaba, ambaye ndiye anaanza kwenye uongozaji wa filamu huku mwandishi mkuu wa filamu hiyo akiwa ni Abigail Arunga, anayejulikana kwa nyimbo za ‘Junior’, ‘Pepeta’ na ‘Lies that Bind’.



