Ligi Ya WanawakeNyumbani
FIFA yaipongeza JKT Queens ubingwa bara

RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) Gianni Infantino ameipongeza JKT Queens kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya soka Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2022/2023.
Ametuma pongezi hizo kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).
“Hilo lisingeweza kufikiwa bila ya bidii ya timu nzima, ari na kujitolea na kila mtu kwenye klabu anaweza kujivunia,” amesema Infantino.
JKT Queens imetwaa ubingwa wa ligi hiyo Mei kwa kufikisha pointi 46 baada ya michezo 18.




