La Liga

Fermín Lopez nje wiki mbili

BARCELONA: KIUNGO wa mabingwa watetezi wa LaLiga FC Barcelona, Fermín López, atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili baada ya kupata jeraha la mguu, klabu hiyo imethibitisha.

Iwapo makadirio hayo yatabaki vilevile, Fermín atakosa mechi nne, ikiwemo ya LaLiga dhidi ya Atletico Madrid wiki ijayo na mechi muhimu ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Eintracht Frankfurt Desemba 9.

Barcelona imesema kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 amepata jeraha dogo katika sehemu ya chini ya mguu wake wa kulia, siku mbili baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Fermín alianza katika mechi hiyo na alicheza kwa zaidi ya dakika 60 kabla ya kutolewa.

Fermín López, ambaye amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu, amefunga mabao saba na kutoa pasi nne za mabao katika mashindano yote. Pia alichangia kuipeleka timu ya taifa ya Hispania kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026.

Related Articles

Back to top button