
KLABU ya Azam imetangaza rasmi kuwa kiungo Feisal Salum ni mchezaji halali wa klabu hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya sakata la muda mrefu kuhusu hatma ya Feisal kufuatia mgogoro wa kimkataba na klabu yake ya zamani, Yanga.

“Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na nyota wa kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum (@feisal194),” imesema Azam kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram.
Kiungo huyo maarufu kama Fei Toto, anakuwa mchezaji wa kwanza kumsajili Azam kuelekea msimu ujao.
Azam imemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na uongozi wa Yanga kwa kuweka wepesi na kufanikisha usajili huo.