EPL

FA yafuta kadi nyekundu ya Evanilson

BOURNEMOUTH:SHIRIKISHO la Soka la Uingereza (FA) limemfutia Mshambuliaji wa AFC Bournemouth, Raia wa Brazil Evanilson kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya Manchester United na sasa ameepuka adhabu ya kufungiwa mechi tatu baada ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England kushinda rufaa waliokata dhidi ya kadi hiyo nyekundu.

M’Brazil huyo mwenye miaka 25 alitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati Bournemouth ilipotoka sare ya 1-1 na Manchester United Jumapili iliyopita dakika ya 70 baada ya VAR kupitia rafu aliyomchezea beki wa kulia wa United Noussair Mazraoui kutengua kadi ya njano aliyopewa na kupewa nyekundu.

Evanilson, ambaye amefunga mabao 11 katika mechi 31 za mashindano yote msimu huu, angekosa mechi za ligi dhidi ya Arsenal, Aston Villa na Manchester City kabla ya kadi yake nyekundu kufutwa.

“Tume huru ya udhibiti imeondoa marufuku ya Evanilson ya mechi tatu kufuatia rufaa ya Bounermouth waliodai mchezaji huyo aliondolewa kimakosa,” FA ilisema katika sehemu ya taarifa iliyotolewa mapema leo. Taarifa hiyo ni afueni kwa Bournemouth walio nafasi ya 10 kwenye Ligi ambao watamjumuisha Evanilson kwenye safari kuelekea Emirates kuwavaa Arsenal Jumamosi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button