EPLKwingineko

FA kuchunguza Bruyne kurushiwa vitu

Chama cha Soka England(FA) kimeanza uchunguzi baada ya kiungo wa Manchester City Kevin De Bruyne kurushiwa vitu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu(EPL) timu hiyo ilipoichapa Arsenal mabao 3-1.

Kiungo huyo alirsushiwa vitu hivyo wakati akitoka uwanjani baada ya kutolewa.

Habari zimesema mwamuzi aliyechezesha mchezo huo Anthony Taylor anaaminika kuorodhesha tukio hilo kwenye ripoti ya mchezo huo.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ameweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii akiwa uwanja wa Emirates na kuandika ‘bia mtu yeyote’?

Katika picha nyingine kinaonekana kikombe kikiwa hewani karibu na Bruyne na ameandika ‘asante!’

Arsenal inachunguza picha za CCTV na imesema itaweka vikwazo vikali iwapo waliojihusisha na tukio hilo watabainika.

“Hii haikubaliki na haitavumiliwa,” ameongeza msemaji wa washika bunduki hao.

De Bruyne alifunga bao na kusaidia lingine wakati City iliposhika uongozi wa EPL kutoka kwa Arsenal baada ya ushindi huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button