EPLKwingineko

Perisic nje msimu mzima

WINGA wa Tottenham Ivan Perisic anatarajiwa kukosa michezo yote ya timu hiyo iliyobaki msimu huu baada ya kupata majeraha ya goti.

Klabu yake imethibitisha kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia mwenye umri wa miaka 34 na uzoefu mkubwa amepata majeraha hayo wakati wa mazoezi bila kuguswa.

Anatarajiwa kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake la kulia kabla ya kuanza matibabu Kaskazini ya London.

Perisic alijiunga na Tottenham kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Inter Milan mwaka 2022 na mkataba wake unatarajiwa kumalizika Julai, 2024.

Spurs haijapoteza mechi katika michezo mitano ya Ligi Kuu England msimu huu chini ya Kocha mpya Ange Postecoglou ikishinda mitano na kutoka sara mmoja.

Related Articles

Back to top button