BurudaniFilamu

Enter the Dragon

HEBU turudi zamani kidogo katika enzi za ubwawa huu na tuangalie kazi ya darekta Robert Clouse ya Enter The Dragon.

Moja ya kazi zenye akshenui kibao na stori kidogo zikishirikisha Bruce Lee, Jim Kelly na John Saxon.

Umaarufu wake Bruce Lee unatokana na filamu nne tu alizotengeneza akiwa mtu mzima na Enter the Dragon ilikuwa kigongo kikali mpaka leo inapendeza kuiangalia.

Filamu hii iliingia thieta mwezi mmoja baada ya kifo chake na kuwa moja ya filamu kali iliyo juu hadi leo.

Ni sinema ambayo inaendelea kung’ara mpaka leo ingawa wadau wanasema wakatik wa utengenezaji wake ilikuwa balaa tupu kutokana na kitu kinaitwa ubabaishaji wa kiufundi wa darekta wake Robert Clouse.

Pamoja na mfadhaiko huo kitu hiki kimegeuka kuwa kitu na boksi kutokana na jinsi watu walivyoipokea Enter the Dragon.

Sinema hii ilimgeuza Bruce Lee kama kiumbe cha kuogofisha kisichozungumza na kikatili na kuwa na uhai pale anapopigana.

Darekta alifanya sinema hii kuwa na watu wasiotaka mzaha hata kidogo kwani hata uigizaji wa Jim Kelly ulikuwa ni mgumu usiokuwa na simile na polisi wabaguzi huku John Saxon akiwa na zile tabasamu za uuaji.

Angela Mao, mdada wa Bruce anafanya vitu vitamu ambavyo vinakufanya ujisikie raha huku Sammo Hung mwenye umri wa miaka 21 na kikosi chake (yuko na Jackie Chan) wakiwa wanachachawa.

Shih Kien aliye na uzoefu wa zaidi ya miaka 30 ni kikaragosi cha Han (adui) ambaye anafanya visa vinavyomfanya Bruce aingie mtamboni.

Ndani unamkuta Bolo Yeung aliyejaza misuli naye akiwa kama msimamizi wa Han.

Sinema hii imejaa mambo magumu na ndipo unapoweza kusema kwamba hakuna mtu katika mapigano ya kujihami anayefanya vyema kama Bruce.

Related Articles

Back to top button