BurudaniMuziki

Duma bado alalamikia mkono wake

MWIGIZAJI wa filamu nchini Daudi Michael ‘Duma’ amesema ilibidi kufanyiwa upasuaji
katika mkono wake ambao ulionekana kuanza kuoza baada ya kushindiakana kupona kwa
dawa za kawaida.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti la HabariLeo, amesema mwanzo alipotangaza mkono wake umeanza kuoza ndani ya siku tatu anasema kuna baadhi ya watu walimuona kama anatafuta kiki, mpaka alipoonesha tobo alilofanyiwa upasuaji.

Amesema anaamini sio ugonjwa wa kawaida kwakuwa hakuwa na dalili za homa wala maumivu, ndiyo maana baada ya kufanyiwa huo upasuaji aliamua kuweka wazi kitendo anachofanyiwa.

“Sisi waigizaji hatupendani tofauti na wanamuziki, yaani naugua hadi mkono unaoza lakini
kuna watu wanajua nafanya utani” amesema.

Duma amesema kama kuna mtu haamini kile ambacho kimemtokea, yupo tayari akamuoneshe mkono wake ulivyo na upasuaji aliofanyiwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button