Mastaa

Drake acheza kamari Ligi Kuu India inayoisha leo usiku

INDIA:WAKATI timu ya Royal Challengers Bangalore (RCB) wakiwania taji lao la kwanza la Ligi Kuu ya India (IPL) leo usiku Juni 3, 2025 katika fainali kali dhidi ya Punjab Kings (PBKS), rapa wa Canada Drake amejiunga nao na kuweka dau la dola 750k kwa ajili ya Bangalore kushinda.

Fainali hiyo ya mchezo wa Kriketi 2025 itachezwa kati ya RCB inayoongozwa na Rajat Patidar na RCB ya Shreyas Iyer kwenye Uwanja wa Narendra Modi mjini Ahmedabad leo usiku huku watu mbalimbali maarufu wakiweka madau mbalimbali ya kamari katika fainali hiyo akiwemo Drake.

Mashabiki wa rapa huyo wa Amerika Kaskazini walishangazwa alipoweka fedha nyingi kwenye mchezo wa kriketi, mchezo ambao haupendwi na watu wengi katika bara analotoka. “Oh! Tuweke kamari kwenye kriketi sasa?” alisema Drake.

Wataalamu wanatabiri kuwa zaidi ya dola bilioni moja zimewekwa kama dau kwenye IPL mwaka huu, duniani kote, huku mashabiki wakiweka kamari kila kitu kuanzia matokeo ya mechi na wafungaji bora hadi matokeo ya kila utoaji. Fainali hiyo itazalisha mamia ya mamilioni ya dola katika mapato ya kamari.

Drake leo katika ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya jinsi alivyoweka dau la dola750k kwenye RCB kushinda IPL 2025 huku risiti yake ikionesha kama atashinda atavuna dola milioni 1.75, na atavuna dola milioni 1.312 ikiwa timu ya Virat Kohli PBKS itaishinda usiku wa leo.

Mmiliki wa timu ya Punjab Preity Zinta anatarajiwa kuwa Uwanja wa Narendra Modi, pamoja na mwigizaji RJ Mahvash, aliyemchumbia mwana spinner wa PBKS Yuzvendra Chahal. Anushka Sharma, mke wa Virat Kohli, naye atakuwa shuhuda wa fainali hiyo itakayopigwa katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu 125,000.

Related Articles

Back to top button