Ligi KuuNyumbani

Dodoma Jiji kujinasua mkiani leo?

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili katika mikoa ya Arusha na Mwanza.

Dodoma Jiji inayoshika nafasi ya 16 mwisho wa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 8 ni wageni wa Polisi Tanzania katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya 15 ikiwa na 5 baada ya michezo 9.

Katika mchezo wa mwingine nyasi za uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza zitawaka moto wakati Kagera Sugar itakapoikaribisha KMC.

KMC ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 9 wakati Kagera Sugar inashika nafasi 13 ikiwa na pointi 8 baada ya mchezo 9.

Related Articles

Back to top button