Diddy anadaiwa kuhifadhi orodha ya maadui wake akiwemo 50 Cent

NEW YORK: RAPA Sean ‘Diddy’ Combs mwenye umri wa miaka 55, anaendelea kukabiliwa na shuhuda mbaya huku kesi yake ya ulanguzi wa ngono ikiendelea mjini New York kufuatia mapumziko ya Siku ya kumbukumbu.
Capricorn Clark ambaye ni msaidizi wa zamani wa Combs, Jana Mei 27, 2025 alitoa ushuhuda kwamba Combs anaorodha ya maadui wake ambao ni watu mashuhuri, akiwemo Suge Knight na Curtis Jackson anayejulikana zaidi kama 50 Cent.
Aliongeza kuwa alimsikia Combs akijadiliana kuhusu bunduki wakati wa mazungumzo kuhusu 50 Cent, muda mfupi baada ya tukio la waandishi wa habari kwenye MTV.
Capricorn aliiambia mahakama: “Alisema, ‘Sipendi nyuma na mbele, sipendi hivyo. Ninapenda bunduki.”
Wakati Combs amekana hadharani kuwa na ugomvi na rapa mwenzake, 50 Cent amekuwa akimkosoa mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii.
Kufuatia ushuhuda wa Clark, rapa huyo alichapisha kwenye ukurasa wa Instagram: “Subiri kidogo PUFFY ana bunduki, siwezi kuamini kuwa sijisikii salama.”
Chapisho hilo liliambatana na picha yake iliyotengenezwa na AI kwenye seti ya filamu.
Combs amekana mashtaka yote yaliyoletwa dhidi yake, sasa kesi yake, ambayo ni wiki ya tatu, imeshuhudia ushuhuda kutoka kwa mashahidi wengi, wakiwemo wafanyikazi wa zamani, wasanii na washirika wake wa karibu.
Scott Mescudi mwenye miaka 40, anayejulikana kama Kid Cudi, tayari ametoa ushahidi kwamba Combs alivunja nyumba yake ya Hollywood Hills mnamo 2011 baada ya kugundua kuwa alikuwa akichumbiana na mwimbaji Cassie Ventura.
Alidai wiki kadhaa baadaye, gari lake lilichomwa moto na akaiambia mahakama: “Ni wazi ilikuwa mbinu ya vitisho.”
Naye Dawn Richard mwenye miaka 40, mwanachama wa zamani wa kikundi cha wasichana Danity Kane, na Cassie Ventura, 37, mshtaki mkuu wa kesi hiyo, pia wametoa ushuhuda unaohusisha Combs kudhibitiwa na tabia ya ukatili.
Timu ya wanasheria ya Combs inashikilia kuwa hana hatia ya ulanguzi wa ngono au ulaghai.
Majina mengine mashuhuri yaliyotajwa kufikia sasa wakati wa kesi yake ni pamoja na Michael B Jordan (37), Barack Obama (62) na Britney Spears (42), ingawa hakuna hata mmoja wao aliyeshtakiwa kwa makosa yoyote.
Kesi inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani huko Manhattan, huku Combs akikabiliwa na kifungo cha maisha jela ikiwa atapatikana na hatia.