Muziki

Davido: Don Jazzy, D’Banj walinifanya niingie kwenye muziki

LAGOS: MSANII nyota wa Nigeria, David Adeleke ‘Davido’, amefichua kuwa wasanii wakongwe Don Jazzy na D’Banj ndio waliompa msukumo wa kuingia kwenye muziki.

Akizungumza katika mahojiano, Davido amesema akiwa na umri wa miaka 14 alishuhudia namna wawili hao walivyofanikiwa kufikisha muziki wa Afrika nje ya mipaka ya bara hili.

“Niliona wakishirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Kanye West na Snoop Dogg, jambo lililonishangaza na kunivutia sana kuona muziki wa Afrika unavuka mipaka,” alisema Davido.

Ameongeza kuwa hatua kubwa waliyopiga Don Jazzy na D’Banj ndio iliyompelekea kufanya uamuzi wa kurudi Nigeria kutoka Marekani, ili kuanza safari yake ya muziki.

Davido kwa sasa ni miongoni mwa mastaa wakubwa barani Afrika, akiwa na mashabiki mamilioni na mafanikio makubwa kwenye majukwaa ya kimataifa.

Kwa upande wa wasanii wa Bongo imekuwa ni kitu kingumu mtu kumtaja aliemshika Mkono nini maoni yako.

Related Articles

Back to top button