Chumba cha Messi Qatar kuwa makumbusho
						CHUMBA alichokuwa akiishi Lionel Messi wakati wa michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar kinatarajiwa kubadilishwa kuwa makumbusho baada ya mafanikio ya Argentina katika michuano hiyo.

Timu ya taifa ya Argentina iliamua kuishi Chuo Kikuu cha Qatar badala ya hoteli za starehe kama zilivyofanya timu timu za nchi nyingine wakati wa michuano hiyo.
Messi alikuwa sehemu muhimu ya taifa lake kutwaa ubingwa wa dunia baaada ya miaka 36 na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo akifunga mabao mawili katika mchezo wa fainali dhidi ya Ufaransa.
Argentina ilishinda kwa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Ufaransa Disemba 18 baada ya sare ya 3-3 muda wa nyongeza na kutwaa ubingwa.
Messi mwenye umri wa miaka 35 alitwaa kiatu cha fedha baada ya kufunga mabao 7 katika michuano hiyo.
Argentina ilianza fainzali hizo za Kombe la Dunia kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Saudi Arabia lakini ikashinda michezo miwili iliyofuata ya kundi lake ikizifunga Mexico na Poland.
				
					



