Ligi KuuNyumbani

Chirwa awatuliza mashabiki Ihefu

MSHAMBULIAJI wa Ihefu, Obrey Chirwa amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwa watulivu wakati wachezaji wakipambana kuendeleza furaha iliyoanza katika klabu hiyo.

Akizungumza na Spotileo, mshambuliaji huyo amesema kuanza msimu vibaya kulitokana na kutozoeana lakini sasa tayari wamechangamka.

“Mashabiki wetu hawapaswi kukata tamaa hii ni ligi tumeanza vibaya kwa sababu za msingi lakini hivi sasa tumeshazoea ni zamu yao kufurahia,” amesema Chirwa.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu Yanga, Azam na Namungo amesema lengo la wachezaji ni kuendelea kupambana ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zijazo za ligi kuu.

Oktoba 16 Ihefu ilipata ushindi wake wa kwanza tangu kuanza msimu huu kwa kuifunga Dodoma Jiji mabao 2-0 na kufikisha pointi tano katika michezo 7 ya ligi iliyocheza.

Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu mchezo unafuata wa Ihefu utakuwa Oktoba 24 dhidi ya Singida Big Stars.

Related Articles

Back to top button