Chelsea yataka dili la kudumu la Lukaku

TETESI za usajili zinaonesha klabu ya Chelsea ina tumaini kukamilisha dili la mkopo wa mshambuliaji Romelu Lukaku katika klabu ya Roma kuwa mpango wa kudumu majira yajayo ya kiangazi.(Standard)
Kylian Mbappe amesema hatma yake katika klabu ya Paris Saint-Germain itatatuliwa ‘siku moja’ huku Real Madrid ikiendelea kuhusishwa na uhamisho huru wa mchezaji huyo.(Telefoot)
Barcelona huenda ikatuma ombi kumsajili kiungo wa Tottenham ambaye kwa sasa sio mchezaji pendwa, Giovani Lo Celso wakati ikitafuta kujaza pengo lilioachwa na Gavi aliyepata majeraha ya muda mrefu. (Mundo Deportivo)
Beki wa kati wa Juventus na Brazil, Gleison Bremer ana nia kujaribu uwezo wake Ligi Kuu England.(Telegraph)
Inter Milan inafuatilia hali za Guido Rodriguez wa Real Betis na Khephren Thuram wa Nice. (Rudy Galetti)
Manchester City imewasiliana na Fluminense ya Brazil kuhusu kinda anayechipukia Matheus Reis mwenye umri wa miaka 16, ambaye anaaminika ana kipengele cha kuachiwa katika mkataba wake cha pauni milioni 44. (Calciomercato)