Osimhen kubadilishana na wawili Arsenal

TETESI za usajili zinasema Napoli imeripotiwa kwa a shauku kusajili nyota wawili Arsenal, hatua inayoonekana inaweza upunguza bei ya pauni mil 110 kwa mlengwa wa The Gunners, Victor Osimhen.(football.london)
Klabu ya Al Nassr ya ligi ya kulipwa Saudi Arabia ipo tayari kuwasilisha ombi la pauni mil 128 Manchester United kumsajili nahodha Bruno Fernandes. (CaughtOffside)
Manchester City itashindana na Barcelona kupata saini ya kiungo wa Bayern Munich, Joshua Kimmich. (BILD – Germany)
Real Madrid itamsajili Joselu kwa uhamisho wa kudumu kutoka Espanyol kufuatia kipindi cha mkopo cha msimu mmoja. (The Athletic)
Manchester United inatarajiwa kumpoteza kinda Omari Forson, 19, majira haya ya kiangazi baada ya mchezaji huyo kukataa ofa ya mwisho ya mkataba.(MailOnline)
Martin Zubimendi wa Real Sociedad na Joao Neves wa Benfica ni miongoni mwa wachezaji Arsenal inayolenga kuwasajili sehemu ya kiungo ingawa kufikiwa makubaliano kwa yeyote kati yao hakutakuwa ka moja kwa moja. (The Athletic)
Tayari Man Utd imewasilisha ombi la pauni mil 51 kumsajili Neves, ambalo Benfica imelikataa. Miamba hiyo ya Ureno inataka ada ya angalau pauni mil 85. (Record – Portugal)