Tetesi

Chelsea kuongeza dau kwa Caicedo

RIPOTI ya mtandao wa Telegraph nchini Uingereza inaeleza Chelsea wanafikiria kuongeza dau kwa kiungo Moises Caideco kutoka Brighton.

Kiungo huyo raia wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21 aliachwa kwenye kikosi cha Seagulls katika mchezo wa kirafiki dhidi Rayo Vallecano.

Awali Chelsea iliwasilisha kwa Brighton ofa ya pauni milioni 70 ikakataliwa, baadaye ikarudi na ofa ya pauni milioni 80 ikakataliwa tena.

Chelsea inaendelea kupambania usajili wa mchezaji huyo ili kuimarisha eneo la kati, hata hivyo nguvu ya Chelsea ni baada ya baadhi ya klabu kujiondoa katika mbio hizo ikiwemo Arsenal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button