Chelsea kupanda dau kwa Caicedo
KLABU ya Chelsea’The Blues’ inakusudia kuipiku Liverpool The Reds’ katika ofa ya kumsajili kiungo wa Brighton & Hove Albion Moises Caicedo, tovuti ya michezo 90min imesema.
The Reds ilikubali kulipa ada ya kuvunja rekodi England ya pauni milioni 111 sawa na shilingi bilioni 341.2 kwa Brington mapema leo na ilitarajia kukamilisha dili la usajili wa kiungo huyo mwisho wa wiki hii.
Caicedo alitarajiwa kwenda makao makuu ya Liverpool, Merseyside kufanyiwa vipimo vya afya leo asubuhi lakini hakwenda na klabu hiyo inaaminika kukasirishwa na mawakala wake.
Habari zinasema nyota huyo wa kimataifa wa Ecuador ameiambia Brighton kwamba anapendelea kuhamia Chelsea na anataka klabu iruhusu muda zaidi kupokea ofa itakayokubalika.
Ofa za Chelsea zenye thamani ya pauni milioni 70 na 80 kwa ajili ya kumsajili Caicedo zilikataliwa na Brighton mapema majira haya ya joto licha kufahamika ofa inayozidi pauni milioni 100 ndio itakayofiriwa na sasa The Blues inataka kuipiku ofa ya Liverpool katika saa chache zijazo ili kujaribu kumaliza dili.




