Featured

Cheche Kocha Mkuu Pan African

UONGOZI wa klabu Pan African ya Dar es Salaam umetambulisha benchi jipya la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Iddy Cheche.

Taarifa ya Ofisa Habari na Mawasiliano wa Pan African inayoshiriki ligi ya Championship, Leen Essau imemtaja Kocha Msaidizi kuwa ni Daudi Macha huku Kocha wa makipa akiwa ni Seif Salum.

“Tunapenda kuwaomba mashabiki, wanachama na wapenzi wa Pan African wampe ushirikiano kocha Cheche katika majukumu yake mapya,”imesema taarifa hiyo.

Cheche aliwahi kukinoa kikosi cha Azam akiwa Kocha Msaidizi pia Kaimu Kocha Mkuu kwa nyakati tofauti.

Related Articles

Back to top button