Habari Mpya

“Chama ni mtu na nusu” – Gamondi

DAR ES SALAAM: WAKATI Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi akiwafungia kazi washambuliaji wake huku akisifia kiwango cha kizuri kilichoonyeshwa na kiungo mshambuliaji, wa timu hiyo Clatous Chama.

Chama Jumamosi, Agosti 17, 2024 alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’o kwa kufunga bao na kutengeneza nafasi ya bao, Yanga ikishinda mabao 4-0.

Gamondi amesema kuwa Chama ni mchezaji mzuri na mzoefu wa michuano ya Afrika licha ya kucheza kwa presha kubwa ilipo juu kulingana na mechi yake ya kwanza kuanza kikosi cha kwanza.

Amesema kila mchezaji ana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwa sababu wana kikosi imara na wachezaji bora katika maeneo yote uwanjani kitu ambacho amekitengeza kwenye timu iwe kwenye kipindi kiruefu na kifupi.

“Mashabiki watarajie makubwa kwa mchezaji huyo kuwepo ndani ya Yanga ni muhimu kulingana na mahitaji ya timu hiyo na malengo ya kushinda mataji mbalimbali wanayoshiriki,” amesema Gamondi.

Amesisitiza kuwa bado anakazi ya kufanya kwenye safu ya ushambuliaji kuhakikisha wanatumia nafasi wanazopata ili kuendelea kufanga idadi kubwa ya mabao.

“Mechi iliyopita tulitengeneza nafasi nyingi, kama tunauwezo wa kushinda mabao zaidi tushinde, tunatakiwa kutumia nafasi tunazotengeneza,” amesema Gamondi na kuwasisitizia washambuliaji wake wanapopata wa kumfunga bao nyingi watumie nafasi vizuri.

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button