EPL

Calafiori afichua maujanja ya Arteta

MILAN, Beki wa Arsenal, raia wa Italia Ricardo Calafiori amefichua mbinu ambazo kocha wa Arsenal Mikel Arteta alitumia kumshawishi kujiunga na Washika mitutu hao wa jiji la London, akisema kuwa meneja huyo alitumia njia zisizo za kawaida kunasa saini yake.

Akizungumza na podcast ya Undici nchini Italia kalafiori amesema njia zilizotumiwa na kocha huyo ikiwemo kumtumia picha ya familia yake ni vitu vilivyochangia sana yeye kutua viunga vya Emirates

“Nilishangazwa sana na namna (Arteta) alivyoonesha kujali kuhusu kunifahamu. Siku moja alinitumia baadhi ya picha za familia yangu kwenye simu na akaniuliza kila mmoja ana thamani gani kwangu”

“Niliguswa sana kwakuwa kitu kama hiki hakikuwahi kutokea katika maisha yangu ya uchezaji. Sisemi kwamba alitumia njia hii pekee ila ni moja ya vitu vilivyonigusa sana na iliashiria matukio muhimu sana kwenye maisha yangu” amesema

Calafiori amekuwa mchezaji muhimu kwenye ukuta wa Arsenal msimu huu ambao klabu hiyo inaendelea kutoa changamoto kwenye mbio za ubingwa akikiwasha kwenye michezo 17 na akiimarika kila kukicha.

Beki huyo kwa sasa yupo na timu yake ya taifa ya Italia inatakayokuwa dimbani Giuseppe Meazza jijini Milan leo saa 4:45 usiku kuwakaribisha wababe wa Ulaya Timu ya taifa ya Ujerumani.

Related Articles

Back to top button