Europa
Busquets kusepa Barcelona

BAADA ya miaka 18, imethibitishwa kiungo wa Barcelona, Sergio Busquets ataondoka klabuni hapo mwisho mwa msimu huu, taarifa ya Fabrizio Romano, mwandishi wa habari wa zamani wa Sky Sport imeeleza kuwa huenda kiungo huyo akasepa Saudia Arabia.
Busquets alijiunga na timu hiyo akitokea timu ya vijana ya ‘Barcelona B’ mwaka 2008.
Tangu aliojiunga na timu hiyo kiungo huyo raia wa Hispania ameshinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara 3, FIFA Club World Cup mara 3, La Liga mara 8 , UEFA Super Cup mara 3, Copa Del Rey mara 7, Spanish Super Cup mara 7.
Mkataba wa Busquets unaisha msimu huu hivyo atakondoka bure kwenda katika klabu nyingine.