Habari Mpya
Bruno yupo sana United

MANCHESTER: BRUNO Fernandez, nahodha wa Manchester United amesaini mkataba mpya utakaomuweka Old Trafford hadi 2027.
Mkataba wa Mreno huyo una kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja hadi 2028. Bruno atakuwa miongoni mwa wachezaji watatu anayelipwa zaidi klabuni hapo.
Bruno alikuwa akilipwa pauni 240,000 tangu kuwasili kwake akitokea Sporting CP ya Ureno mwaka 2020.
Kwa sasa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo ni Casemiro anayechukuwa pauni 350,000 kwa wiki akifuatiwa na Marcus Rashford anayelipwa 300,000.