EPLKwingineko

Bournemouth yamtimua kocha

KLABU ya Bournemouth imemmfukuza kazi Kocha Scott Parker michezo minne tu baada msimu wa Ligi Kuu Uingereza kuanza.

Parker ambaye ameipandisha raraja timu hiyo kutoka Championship msimu uliopita imefungwa michezo mitatu ya mwanzo wa msimu kikiwemo kichapo cha mabao 9-0 kutoka kwa Liverpool Agosti 27.

Gary O’Neil atakuwa kocha wa muda wa timu hiyo na tasaidiwa na Shaun Cooper na Tommy Elphick.

“AFC Bournemouth inatangaza kuwa klabu imeachana na Kocha Mkuu Scott Parker,” taarifa imesema katika tovuti ya klabu.

Mmiliki wa Bournemouth Maxim Demin amesema: “Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Scott na timu yake kwa juhudi zao wakati wakiwa nasi. Kupanda kwetu daraja hadi Ligi Kuu msimu uliopita chini ya uongozi wake kutakumbukwa daima kama moja ya misimu ya mafanikio zaidi katika historia yetu.”

Bournemouth ilipoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Manchester City, na ikafungwa mabao 3-0 na Arsenal.

Related Articles

Back to top button